Kitabu hiki, Pemba: Muhanga wa Siasa, kinajaribu kwa mara ya kwanza
kabisa kuchambuwa tatizo la ubaguzi wa kijamii ambalo huwa halisemwi kwa
uwazi ndani ya visiwa vya Zanzibar, na ambalo chimbuko lake ni dhana
potofu na matokeo yake ni ubomolewaji wa misingi ya taifa hili la visiwa
vya Bahari ya Hindi, mashariki mwa Afrika.