Historia ya Kiziba na Wafalme Wake: Tafsiri ya Amakuru Ga Kiziba na
Abakama Bamu ni mchango mkubwa kwa fasihi ya kihistoria ya wenyeji wa
Afrika ya Mashariki na Tanzania. Utafiti wa Mfalme Mutahangarwa wa
Kiziba (aliyetawala 1903-1916) katika mwanzo wa karne ya ishirini
ulikusanya mabingwa wa simulizi za mdomo kutoka katika koo za kifalme na
zisizo za kifalme na shuhuda zao ziliandikwa na watu waliokwisha kujua
kusoma na kuandika, akiwemo F.X. Lwamgira. Miongo mine baadaye matokeo
ya utafiti huo yalipigwachapa kikatokea kitabu chenye kurasa 490 katika
lugha ya Kihaya ambach kilibaki bila kujulikana ingawa kilikuwa kitabu
muhimu. Tafsiri hii muhimu itafanya historia ya Kaskazini Magharibi mwa
Tanzania na Kusini Magharibi mwa Uganda kabla na mwanzoni mwa ukoloni
iwafikie kwa mara ya kwanza wasomi wengi.